Hongereni kwa kuchaguliwa "The White University" Nawashauri hivi:-

1. Yapo makampuni ya mabasi yatawataka mlipe pesa benki ili yawasafirishe hadi UDOM- Kataa kwani watakupiga hela
halafu safari utaiona chungu. Hata wakijifanya wameingia mkataba na chuo, usiingie mkenge. Chukua basi kwa
kujitegemea wewe mwenyewe.

2. Stendi ya daladala zote ndani ya Dodoma huanzia safari zake stendi ndogo ya daladala-Jamatini. Kuwa makini na
eneo hilo kwani waleti na simu za mkononi hapo zinasakwa kwa udi na uvumba.

3. Uwe na uhakika wa College unayokwenda. Kwa kifupi, ziko daladala zinazokwenda Education, jina jingine wanapaita
Ng'ong'ona ama Ng'ox. Wale waliochaguliwa college of Education, Medicine, Informatics na natural Science upande
daladala hizo, vinginevyo utapata tabu kubwa.

4. Wewe unaekwenda College of social science pamoja na humanities panda daladala inayokwenda Social au Bondeni.
Kinyume na hapo utajiju.

5. Nauli kwa daladala ni Tsh 350 kwa safari yoyote ndani ya College, Kutoka Jamatini hadi Chuo ni 350 pia. Wahuni
wanapiga hadi 1500/- kwani wanajua kuwa ni wageni hamjui kitu.

6. Tax inategemea maelewano, standard bei ni elf 8-10. epuka kupanda tax kwani utazungushwa mjini mitaa karibu
yote na watakwambia bei kubwa, hata hivyo, kama huna uhakika wa college yako pia wanaweza kukuingiza ndani
ya chuo wakakuzungusha college zote, watakuchanganya na majengo then watakupiga hela ndefu.

7. (kwa wanaokwenda social science) Chagua mavazi ya heshima kwani ukidhani unakwenda kujiachia unaweza
ukajikuta unarudi nyumbani siku hiyo hiyo, Kwa wanadada, vimini, suruali za kubana, nguo za ajabu ajabu waachie
wadogo zako. Kama huna za kushonesha anza kuzitafuta. Kwa wanakaka, punguza idadi ya majinzi ( Hasa kwa
wanaokwenda social science), mitindo ya kata K, kusuka nywele, kuvaa heleni potezea kwenu.

8. Kama mnasafiri kwa kampani, kuweni makini na College mnazokwenda, ikitokea kwamba mmefika Dodoma na si
wenyeji hivyo kwenda chuoni moja kwa moja, na ikiwa College
zenu ni tofauti mtalazimika kutengana hapo ili kila mmoja apande gari ya college inayomhusu ili kuepusha usumbufu,

9. Wenyeji wenu (mwaka 2na 3) hawapo na mtakuwa wageni watupu eneo hilo, Usimwamini mtu yeyote pahala popote
pale ndani na nje ya College.


Huu ni ushauri wangu kwa uzoefu mdogo nilioupata pindi nilipokuwa huko Idodomiya. Kila la Kheri!