VYUO VYETU TANZANIA

VyuoVyetu Tanzania





Wednesday, December 12, 2012

JOBS KWA WALIO MALIZA CHUO NA VIGEZO

other jobs

Thursday, November 8, 2012

VYUONI KWETU UKOO

tutafika kweliiiii?mwanao/ndugu/rafiki wa kike akishindwa chuo kwa maana akidisco...usijudge mojakwa moja kuwa hasomi kuna mengi kama hayo uya onayooo katika picha....HAKI ELIMU..?

Sunday, October 28, 2012

TUMUOMBEE MTOTO HUYU..JULIANA MWINUKA

JULIA HUYU HAPA siku YA JUMATATUU ALIFANYIWA OPARESHENI CCBRT

Mtoto  Juliana Mwinuka
 
Majeraha  yaliyotokana na kuungua moto klatika  uso wa mtoto  mtoto  Juliana Mwinuka (16) mkazi  wa kitongoji cha Ushindi kata ya Mavanga  wilaya ya  Ludewa  mkoa  wa Njombe yameanza kuziba taratibu huku leo anategemea  kukutana na madaktari bingwa duniani ambao  wamewasili katika Hospitali ya CCBRT .

Kila mmoja  wetu tunaomba aendelee  kumwomba Mwenyezi Mungu kwa  dini yake ili kuweza  kutenda miujiza  ili mtoto  huyo aweze kupona.

 Mtandao huu unaendelea kuwapongeza wote wanaoendelea kuguswa na kuungana na wadau wengine kumchangia fedha za matibabu ,mtoto Juliana kama anavyoonekana akiwa ameunga uso wake kwa moto ni yatima anahitaji msaada wako ili kunusuru maisha yake waweza kutuma mchango wako kwa njia ya M-PESA katika namba hii 0754 026 299 au Tigo Pesa 0712 750199 namba hizi ni za mmiliki wa Bw Francis Godwin

Nawaomba tuungane kufanikisha kuokoa maisha ya mtoto Juliana Mwinuka na Mungu atatuongezea zaidi

Thursday, October 25, 2012

Waliogomea Shahada za UCLAS sasa kutunukiwa na UDSM


Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kitakuwa na mahafali ya 42 tarehe 27 Oktoba 2012 na Novemba 3, 3012.

 Jumla ya wahitimu 3,643 watatunukiwa shahada na stashahada wakati wahitimu 902 wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ardhi (UCLAS) watatunukiwa shahada.

UCLAS kwa sasa ni sehemu ya UDSM.

Hayo yalisemwa na Makamu Mkuu wa wa UDSM, Profesa Rwekaza Mukandala akitoa taarifa kwa umma kupitia waandishi wa habari.

“Tunapenda kuufahamisha umma pia kuwa, katika mahafali ya sasa wanafunzi wa UCLAS na wao watatunukiwa shahada kama wanafunzi wa UDSM, uamuzi huu umefuatia kumalizika kwa kesi Lello & Others Vs Ardhi University, University of Dar es Salaam and Attornry General, Misc.Civil Cause No. 69 of 2008, iliyofunguliwa na wanafunzi wa UCLAS wakipinga kupata shahada za UCLAS kwa madai kuwa udahili wao ulibaki wa UDSM, hivyo UDSM kinakubalina kwa dhati na uamuzi wa Mahakama Kuu,” alisema Prof Mukandala.

UDSM imekubali kuwatunuku shahada mbalimbali wahitimu hao 902 waliomaliza masomo yao UCLAS ambao awali waligoma kutunukiwa shahada zao na chuo hicho (UCLAS) katika Mahafali ya 42 kutokana na madai kuwa walipata udahili chini ya UDSM wakati UCLAS kilipopata hadhi ya kuwa chuo kikuu kinachojitegemea mwaka 2007 hivyo walistahili kutunukiwa shahada na chuo kilichowadahili. Wanafunzi hao ni wale waliohitimu masomo katika miaka ya 2007 hadi 2010.

Wanafunzi hao kwa kupinga suala hilo walifungua kesi mahakamani dhidi ya Chuo Kikuu cha Ardhi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

“Sisi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tumekubaliana kwa dhati na uamuzi huu wa mahakama na tumeamua kuwatunuku shahada wanafunzi hao kwa vile hakuna rufaa iliyokatwa dhidi ya uamuzi huo,” alisema Profesa Mukandala.

Kati ya watakaotunukiwa shahada mbalimbali, 28 watatunukiwa Shahada za Uzamivu, 671 Shahada ya Uzamili; 153 Stashahada za Uzamili na 2, 790 Shahada ya Kwanza.

Licha ya mahafali hayo, Profesa Mukandala alisema chuo hicho kitahitimisha maadhimisho ya miaka 50 ya kuanzishwa kwake kwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwamo kufanya mkutano na wahitimu waliowahi kusoma chuoni hapo shughuli ambayo itafanyika Alhamisi.

Profesa Mukandala alisema wakati wa kuhitimisha sherehe hizo, shughuli zitakazofanyika ni kuweka jiwe la msingi la jengo la kituo cha wanafunzi, kuzindua Dira ya Chuo hicho (UDSM Vision 2061) na kutoa tuzo mbalimbali kwa watu na vikundi vilivyotoa mchango uliotukuka kwa chuo kikuu katika miaka 50 iliyopita.

Akizungumzia dira hiyo, alisema itakuwa ni ya nusu karne ijayo na malengo yake ni kufikia mwaka 2061 chuo kitakuwa katika nafasi za juu za viwango vya ubora vya kimataifa.

---
Habari via Nipashe  na DHabariLeo

Wednesday, October 24, 2012

MKUTANO WA KWANZA WA UMOJA WA VYUO VIKUU ELIMU YA JUU VYA AFRIKA MASHARIKI

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua mkutano wa kwanza wa Umoja wa Vyuo Vikuu  unaoshirikisha pia Kamisheni ya Biashara ya Afrika Mashariki. Mkutano huo unafanyika kwa siku tatu jijini Arusha na unajumuisha wakuu na wawakilishi wa vyuo mbalimbali vya elimu ya juu katika ukanda wa Afrika Mashariki.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Mwenyekiti wa Umoja wa Mawaziri wa Afrika Mashariki, Musa Sirima, wakati wa uzinduzi wa mkutano wa kwanza wa Umoja wa Vyuo Vikuu  unaoshirikisha pia Kamisheni ya Biashara ya Afrika Mashariki. Mkutano huo unafanyika kwa siku tatu jijini Arusha na unajumuisha wakuu na wawakilishi wa vyuo mbalimbali vya elimu ya juu katika ukanda wa Afrika Mashariki.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Makamu Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Augustine, Dkt. Charles Kitima, wakati alipokuwa akitembelea kukagua mabanda ya maonyesho baada ya kufungua mkutano wa kwanza wa Umoja wa Vyuo Vikuu  unaoshirikisha pia Kamisheni ya Biashara ya Afrika Mashariki. Mkutano huo unafanyika kwa siku tatu jijini Arusha na unajumuisha wakuu na wawakilishi wa vyuo mbalimbali vya elimu ya juu katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano wa kwanza wa Umoja wa Vyuo Vikuu  unaoshirikisha pia Kamisheni ya Biashara ya Afrika Mashariki. Mkutano huo unafanyika kwa siku tatu jijini Arusha na unajumuisha wakuu na wawakilishi wa vyuo mbalimbali vya elimu ya juu katika ukanda wa Afrika Mashariki. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

Sunday, September 23, 2012

UDOM;IMPORTANT NOTICE TO FIRST YEAR AND CONTINUING STUDENTS


NEWS AND ANNOUNCEMENTS 

NJIA RAISI ZAIDI YA KUWEZA KUONA KAMA UMEPATA MKOPO.

NJIA RAISI ZAIDI YA KUWEZA KUONA KAMA UMEPATA MKOPO..TUUNGANE PAMOJAAA
Welcome to HESLB
First Year Loans Allocation Results
Written by Administrator
Thursday, 20 September 2012 06:03
Thank you for your patience while our technical experts were solving technical glitches in our servers. Loans Allocations for First Year students for Academic Year 2012/13 are now available in our website. Click the following link to access the site with the results (N.B: Please allow popup blocker in your browser) View Results

Wednesday, September 19, 2012

BAADHI YA WALIOPATA MKOPO 2012/2013 VYUONI


           BAADHI YA WALIOPATA MKOPO 2012/2013 VYUONI,,,CLICK KUTAZAMA


                                       6: 2012/13 Loans Allocations List 4-A (SU - TU)
                                        7: 2012/13 Loans Allocations List 4-B (TU -UDOM)
                                        8: 2012/13 Loans Allocations List 5-A (UDOM -UDOM)
                                       9: 2012/13 Loans Allocations List 5-B (UDOM -UDSM)
                                        10: 2012/13 Loans Allocations List 6 (UDSM -ZU)

Saturday, September 15, 2012

IFM-Joining Instructions for Undergraduateand Postgraduate Students (2012/2013) and Acknowledgement Of Admission Offer

Joining Instructions for Undergraduateand Postgraduate Students (2012/2013) and
Acknowledgement Of Admission Offer 

Ushauri wa bure kwa waliochaguliwa udom!


Ushauri wa bure kwa waliochaguliwa udom!

Hongereni kwa kuchaguliwa "The White University" Nawashauri hivi:-

1. Yapo makampuni ya mabasi yatawataka mlipe pesa benki ili yawasafirishe hadi UDOM- Kataa kwani watakupiga hela
halafu safari utaiona chungu. Hata wakijifanya wameingia mkataba na chuo, usiingie mkenge. Chukua basi kwa
kujitegemea wewe mwenyewe.

2. Stendi ya daladala zote ndani ya Dodoma huanzia safari zake stendi ndogo ya daladala-Jamatini. Kuwa makini na
eneo hilo kwani waleti na simu za mkononi hapo zinasakwa kwa udi na uvumba.

3. Uwe na uhakika wa College unayokwenda. Kwa kifupi, ziko daladala zinazokwenda Education, jina jingine wanapaita
Ng'ong'ona ama Ng'ox. Wale waliochaguliwa college of Education, Medicine, Informatics na natural Science upande
daladala hizo, vinginevyo utapata tabu kubwa.

4. Wewe unaekwenda College of social science pamoja na humanities panda daladala inayokwenda Social au Bondeni.
Kinyume na hapo utajiju.

5. Nauli kwa daladala ni Tsh 350 kwa safari yoyote ndani ya College, Kutoka Jamatini hadi Chuo ni 350 pia. Wahuni
wanapiga hadi 1500/- kwani wanajua kuwa ni wageni hamjui kitu.

6. Tax inategemea maelewano, standard bei ni elf 8-10. epuka kupanda tax kwani utazungushwa mjini mitaa karibu
yote na watakwambia bei kubwa, hata hivyo, kama huna uhakika wa college yako pia wanaweza kukuingiza ndani
ya chuo wakakuzungusha college zote, watakuchanganya na majengo then watakupiga hela ndefu.

7. (kwa wanaokwenda social science) Chagua mavazi ya heshima kwani ukidhani unakwenda kujiachia unaweza
ukajikuta unarudi nyumbani siku hiyo hiyo, Kwa wanadada, vimini, suruali za kubana, nguo za ajabu ajabu waachie
wadogo zako. Kama huna za kushonesha anza kuzitafuta. Kwa wanakaka, punguza idadi ya majinzi ( Hasa kwa
wanaokwenda social science), mitindo ya kata K, kusuka nywele, kuvaa heleni potezea kwenu.

8. Kama mnasafiri kwa kampani, kuweni makini na College mnazokwenda, ikitokea kwamba mmefika Dodoma na si
wenyeji hivyo kwenda chuoni moja kwa moja, na ikiwa College
zenu ni tofauti mtalazimika kutengana hapo ili kila mmoja apande gari ya college inayomhusu ili kuepusha usumbufu,

9. Wenyeji wenu (mwaka 2na 3) hawapo na mtakuwa wageni watupu eneo hilo, Usimwamini mtu yeyote pahala popote
pale ndani na nje ya College.


Huu ni ushauri wangu kwa uzoefu mdogo nilioupata pindi nilipokuwa huko Idodomiya. Kila la Kheri!

Sunday, September 2, 2012



 WANAFUNZI 10 MWAKA WA 5 UDAKTARI (MEDICINE) MUHIMBILI UNIVERSITY WALIOKUWA DISCONTINUED


Wakuu, kuna wanafunzi 10 waliomaliza mwaka wa 5 fani ya medicine (udaktari), wamekuwa discontinued kutokana na tangazo la dean school of Medicine Prof. Karim Manji, source ya kudiscontinue ni kutokusubmit elective report (hii ni research inayofanywa mwaka wa nne). Wanafunzi hao ambao wamemaliza ratiba zao za masomo na ilibidi wa graduate mwaka huu.
Name
sex
Reg no
MIHAYO, Gloria
F
2007-04-00434
ABED, Charles
M
2007-04-00319
SAID, Mbaraka
M
2007-04-00403
MAHUNDI, Salvatory
M
2007-04-00493
NYERERE, Semeni
M
2007-04-00517
RAMADHANI, Said
M
2007-04-00531
MAGESA, Jaralya
M
2007-04-00540
SAID Kizunzi
M
2007-04-00548
SALIM, Mohammed S.A
M
2007-04-00553
MY TAKE: 1: Activist, toeni solution ya jambo hili, inawezekana vipi mtu aliyesoma miaka mitano aje adisco kirahisi kiasi hichi
2: Prof karim manji, ni mtu hatari sana Muhimbili, ameshinikiza maamuzi haya, naomba journalist wafanye utafiti wa jambo hili
3: Wana JamiiPress naombeni tutoe way foward juu ya jambo hili, hasa ni kwa jisni gani linaweza kuwa solved,
4: watu wa Usalama wa taifa fanyeni uchunguzi juu ya jambo hili, hii ni hatari kwa haki wa watanzania wanafunzi walioamua kusoma fani hii ya udaktari kwa miaka mitano then wanadisco kirahisi hivi

MWANAFUNZI CHUO KIKUU MIST MBEYA AVUMBUA KIFAA CHA KUDHIBITI AJALI ZA MELI BAHARINI


MWANAFUNZI CHUO KIKUU MIST MBEYA AVUMBUA KIFAA CHA KUDHIBITI AJALI ZA MELI BAHARINI






Mtaalamu maswala ya umeme Joseph Matwani akiwaelezea baadhi ya wananchi waliotembele banda hilo jinzi kifaa hicho kinavyofanyakazi
MWANAFUNZI wa Chuo kikuu cha sayansi na teknolojia Mbeya (MIST) amebuni  na kutengeneza kifaa maalum kinachodaiwa kuweza kudhibiti kupunguza na ikiwezekana kumaliza kabisa tatizo la ajali za vyombo vya usafiri wa bahari kama ilivyotokea hivi karibuni kwa Meli ya Mv.Skargit iliyogharimu maisha ya watanzania wengi.

Akizungumza na Mbeya yetu Mtaalamu wa masuala ya umeme katika chuo hicho,Joseph Matwani amemtaja mwanafunzi aliyekitengeneza kifaa hicho ambacho kinabaini meli ama boti litakalozidisha abiria ama mizigo  kuwa ni Zuberi Rutumbo.

Bw.Matwani alisema kifaa hicho ambacho bado akijapewa jina kitakuwa na uwezo wa kutoa taarifa katika mamlaka husika mathalani,Sumatra,Polisi,kwa mmiliki,nahodha na mamlaka nyinginezo zitakazoingizwa katika programu maalum kuwa meli Fulani imejaza mzigo kuliko uwezo wake na hivyo kusaidia kuizuia bandarini kabla haijaondoka.

Mtaalamu huyo amesema kuwa kifaa hicho kitafungwa katika vyombo mbalimbali vya usafiri wa baharini  ambapo vitawaonesha makapteni kuona kiasi cha mzigo uliopakiwa na kuwajulisha endapo watazidisha baada ya maji kuvuka mstari wa chombo husikai kabla ya kuondoka na hivyo  kutoa mlio wa taadhari na baada ya sekunde kumia ujumbe unakwenda katika nambari za simu zilizokuwa zimefanyiwa programu katika kadi ya simu
.
Amesema kutokana na taarifa hiyo ya ujmbe mfupi wa maneno katika simu za wahusika wanatumaini kuwa watachukuwa hatua kukizuia chombo hicho kisiondoke na hivyo kufanikiwa kunusuru maisha ya  abiria na kupunguza ajali zinazodaiwa zinasababishwa na uzembe wa makapteni kuzidisha mzigo kwa makusudi.

Mvumbuzi huyo Rutumbo amesema ameamua kutengeneza kifaa hicho alichoanza kukifikiria tangu mwaka 2011  baada ya  kuibuka kwa ajali  mbaya za meli ya Mv.Bukoba,Mv.Spice  na juzi Mv.Skargit na hivyo kuamua kuandika ‘project’ ( mradi) baada ya kushuhudia matukio hayo.

Amesema ajali nyingi zinaonekana zinasababishwa na uzembe wa watu wachache waio na huruma na watanzania lakini anaamini kupitia kifaa hicho uwajibikaji utaongezeka na kila mmoja atawajibika kupitia nafasi yake na kuwabaini wazembe ambapo pia kifaa hicho kinaweza kufungwa  katika mlango ama dirisha katika nyumba na kuprogramu katika simu na hivyo kukupa taarifa ya uhalifu endapo unatokea.

TUNAENDA WAPI JAMANIII..?"UKURASA FACEBOOK UNAOUZA WANA CHUO"



UKURASA FACEBOOK UNAOUZA WANA CHUO

'Campus Divas For Rich Men’ 
  
Jane 18 has just finished high school and will be joining UoN she wants a rich dude who is willing to pay her half % school fees 
“Sisi madiva tuna gharama, NYWELE, zinataka dawa! MASIKIO yanataka,hereni!! MACHO yanataka wanja na shadow! PUA inatka kipini! MDOMO, unatka lipstic! USO unataka poda na foundation! SHINGO inataka cheni! MATITI yanataka sidiria! MIKONO inataka Bangali! VIDOLE vinataka, Pete! KIUNO kinataka shanga. MA***KO yanataka chupi MIGUU inataka hina rangi na viatu. KAMA HUNA MKWANJA POLEEEEEEE,” ni baadhi ya status zinazosomeka kwenye ukurasa uitwao 'Campus Divas For Rich Men’.
Ni ukurasa maarufu sana kwenye Facebook sasa hivi nchini Kenya, ukiwa na likes 34,339. 
Ukurasa huu huonesha picha za wasichana ‘wanaodaiwa kuwa ni wanachuo’ wakijiuza na kutafuta wanaume wenye fedha ili wawatimizie haja zao.
Hata hivyo kwa uchunguzi uliofanywa na gazeti la Daily Post, umegundua mtu aliyeufungua ukurasa huo ambao kiukweli picha na majina anayoyaweka sio vya kweli.
Huyu ndiye aliyeanzisha ukurasa huo
Mtu huyo ni mvulana ambaye inasemekana kuwa alikuwa akimpenda msichana aitwaye Samira Osman lakini alipokataliwa, aliamua kufungua ukurasa huo kwa hasira.
Hivi ndivyo anavyoweka picha za wasichana zikiwa na maelezo kuwa wanataka wanaume matajiri huku maelezo akiyaandika mwenyewe.
 
Candy 20 Kenyatta university wants a rich man who can cater for her needs

MUNGU OKO HII KITU JAMANIIII DAAH..

KILUVYA

KILUVYA
MASHONO

UDOM

UDOM
DODOMA UNIVERSITY