VYUO VYETU TANZANIA

VyuoVyetu Tanzania





Tuesday, February 19, 2013

ROSE MIGIRO ATEULIWA KUWA MKUU WA CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA

ROSE MIGIRO ATEULIWA KUWA MKUU WA CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dkt. Asha Rose Migiro kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Taarifa iliyotolewa Dare Es Salaam na kutiwa saini , Jumatano, Januari 30, 2013 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue imesema kuwa uteuzi huo ulianza Alhamisi ya Januari 17, mwaka huu wa 2013.

Mheshimiwa Asha Rose Migiro ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Katibu wa NEC wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Aidha, Dkt. Migiro amepata kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU
DAR ES SALAAM
30 Januari, 2013

source Aranse blog

Monday, January 14, 2013

KAMANDA KOVA azungumza na Wanafunzi wa IFM

                    Wanafunzi Baada ya kufika Wizara ya Mambo ya ndani  wakimsubiri RPC
 Rais wa serikali ya wanafunzi wa IFM  Michael S.Charse akijaribu kumuelewesha kamanda  KOVA kero inayo wakumba wanafunzi wa Ifm waishio kigamboni.
 Afande KOVA akizungumza na wanafunzi wa IFM pamoja na vyombo vya habari.


Wanafunzi wakielekea kigamboniii woteee kwa nguvu mojaaa tumechoka tumechoka

IFM...YALALAMIKIA UONGOZI JUU YA YANAYOTOKEA KIGAMBONI

 Wanafunzi wa IFM walipo kutana kwa pamoja katika viwanja vya chuoni hapo kabla ya kufikia uamuzi wa kwenda wizara ya mambo ya Mambo ya Ndani.Kupata hitimisho la matatizo ya ujambazi yanayotokea kigamboni kwa wanafunzi hoa, ambapo huibiwa laptop,simu na baadhi ya vitu vyenye thamani. Majambazi/wezi hao huja wengi takribani wanne na mapanga na visu na kuwaacha wanafunzi na majeraha, hali hiyo imekuwa tatizo zaidi kwa muda wa takribani wiki 4 bila chochote kufanyika mpaka imefikia  hatua ya wanafunzi wa kiume kuingiliwa kinyume na maumbilee

Baadhi yaWanafunzi wa IFM wakijaribu kuwasiliana na wanafunzi wenzao kuhusiana na matatizo yaliyotokea

KILUVYA

KILUVYA
MASHONO

UDOM

UDOM
DODOMA UNIVERSITY