VYUO VYETU TANZANIA

VyuoVyetu Tanzania





Sunday, August 19, 2012

BIMA YA AFYA KWA WANACHUO WOTE TANZANIA


Huduma kwa Wanachuo

Utangulizi.
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya pia unasimamia huduma za matibabu kwa Wanafunziwa Vyuo vya Elimu ya juu nchini kote. Utaratibu huu unalenga kuwapa Bima ya Afya wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu popote nchini ambapo mwanafunzi atapata huduma za matibabu wakati atakapokuwa masomoni na wakati wa likizo katika muhula husika.Huduma za matibabu kwa wanafunzi zinapatikana katika Hospitali,Vituo vya Afya, Zahanati na Maduka ya Dawa yaliyosajiliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Tanzania.
Utaratibu wa Kujiunga.
  • Wanafunzi wanaandikishwa chini ya udhaimi wa chuo husika kama Taasisi.
  • Kutakuwa na Mkataba maalumu wa maridhiano kati ya Taasisi husika(Chuo) na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
  • Mkataba kati ya mwanafuni na NHIF ni wa kipindi cha miaka mitatu , ambao unarejewa kila mwaka.
  • Huduma za matibabu kwa wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu hazihusishi wenza wao wala wategemezi.
Michango.
  • Chini ya utaratibu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, mwanafunzi husika anatakiwa kuchangia Shs 4,200 kwa Mwezi sawa na Shs 50,400 kwa Mwaka.
  • Wanafunzi ambao tayari wana vitambulisho vya matibabu vya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, hawatahusika na uchangiaji huu kwa kuwa wao tayari ni wanachama wa Mfuko.
  • Taasisi husika (Chuo) ndiyo yenye dhamana ya kuwasilisha michango ya wanafunzi watakaoandikishwa chini ya utaratibu huu.
  • Michango ya kila mwezi ya wanufaika wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya inatakiwa kuwasilishwa katika Ofi si za Kanda zilizopo karibu.
  • Jinsi ya Kujisajili.
  • Mwanafunzi atajaza fomu ya kujisajili,
  • Atatakiwa kuleta picha mbili za ukubwa wa pasipoti
  • Mwanafunzi atapata kitambulisho cha matibabu ambacho atakitumia kwa ajili ya matibabu.
Mafao yanayotolewa
Wanafunzi wa Vyuo vya ELimu ya Juu waliojiunga na NHIF watanufaika na mafao yote KUMI na MOJA yanayotolewa na Mfuko.
Ikumbukwe kuwa mwanafunzi akishamaliza masomo anawajibika kurejesha kitambulisho cha matibabu cha NHIF kwenye chuo alikojiandikisha

No comments:

KILUVYA

KILUVYA
MASHONO

UDOM

UDOM
DODOMA UNIVERSITY