VYUO VYETU TANZANIA

VyuoVyetu Tanzania





Monday, August 20, 2012

vyuo feki tanzania...jamii inatakiwa kuwa makini

Hii ndiyo orodha ya vyuo vinavayotambulika serikalini. Vyuovisivyokuwemo katika orodha hii ni feki, hivyo jamii inatahadharishwa kuwa makini.


Baadhi ya vyuo vinavyosimamiwa na VETA vimekuwa vikitoamafunzo ya diploma jambo ambalo ni kinyume na taratibu
KILA siku afadhali ya jana! mfumo wa elimu nchini bado unaendelea kugubikwa nachangamoto nyingi kila kukicha kutokana na watu wasio waaminifu kutumia vibayafursa za kuanzisha taasisi za elimu.

Kwa mfano, watu hawa wamekuwa wakianzisha vyuovisivyokidhi matakwa ya kisheria kiasi kwamba sio tu wanafunzi hupata elimuchini ya kiwango, lakini pia wanakosa kutambuliwa na mamlaka husika. 

Uchunguzi wa siku kadhaa wa Mwananchi umebaini pamoja na kujitangaza katika vyombo vyahabari, vyuo vingi vinavyotoa koziza cheti na diploma katika miji mikubwanchini hususan katika jiji la Dar es Salaam, havina sifa na havitambuliwi na mamlaka zinazosimamia elimuya ufundi nchini.

Kwa mujibu wa mfumo wa mafunzo na elimu nchini, Taasisi za elimu ya juu (Tertiary) zisizokuwa vyuo vikuu, zinapaswa kusajiliwana kupewa ithibati na Baraza la Taifa laUsimamizi wa Elimu ya Ufundi (NACTE). 
Aghlabu vyuo hivi ni vile vinavyotoa mafunzo ya kozi zacheti, diploma na baadhi katika miaka ya karibuni vimekuwa vikitoa mafunzo yakozi za shahada ya kwanza.

Mamlaka nyingine ambayo kwa mujibu wa sheria inapaswakusimamia mafunzo ya ufundi hasa kwa vyuo na taasisi zinazotoa mafunzo kwangazi ya cheti pekee ni Mamlaka ya Elimuna Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).

Hata hivyo, kwamujibu wa uchunguzi, wakati vyuo vinavyosimamiwa na NACTE vikiruhusiwa kisheriakutoa mafunzo ya daraja la cheti, imebainika vyuo vingi vya hadhi ya chetivinavyosimamiwa na VETA, navyo vimekuwavikijitangaza na kutoa mafunzo yadiploma, jambo ambalo ni kinyume na taratibu.

Uchunguzi umegundua kuwa vyuo hivi ni vile vinavyotoa mafunzo katika fani za , Uongoziwa Biashara, Menejimenti ya hoteli, Utawala, Uhasibu, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Teknohama), Utalii na Sayansi ya kompyuta.

Vipo pia vyuo vinavyodai kutoa kozi za diploma kwa usajiliwa vyuo vya nje hususan nchini Uingereza 
Kwa mujibu wa NACTE, vyuo vya uhasibu, biashara na utawalavinavyotambuliwa kwa hadhi ya ithibati kamili ni pamoja na Chuo cha Usimamiziwa Fedha (IFM), Taasisi ya Uhasibu Arusha, Chuo cha Elimu ya Biashara Dar esSalaam (CBE), CBE Dodoma, Taasisi ya Uhasibu Tanzania (Dar es Salaam,), Taasisiya Uhasibu Tanzania (Singida), Taasisi ya Uhasibu Tanzania (Mbeya), 

Vingine ni Utumishi Dar es Salaam, Taasisi ya Usimamizi waFedha Zanzibar, Chuo cha Mahakama Lushoto (ithibati ya muda), Utumishi Tabora,Taasisi ya Ugavi na Ununuzi Dar es Salaam (ithibati ya muda), Chuo cha Shukran, Chuo cha Kodi Dar es Salaam, ESAMI(ithibati ya muda) na Hombolo.

Upande wa vyuo vya kategori ya Kilimo, Maliasili naMazingira, kundi linalojumuisha pia vyuo vya utalii, taasisi zinazotambuliwakwa hadhi ya ithibati ni Tengeru, Mbegani, Chuo cha Wanyama Pasiansi, Chuo chaKilimo Uyole, Mweka, Chuo cha Misitu Olmotonyi, Taasisi ya mafunzo ya KilimoMtwara,.

Vyuo vingine ni Taasisi ya Uvuvi Nyegezi, Chuo cha Taifa chaUtalii, Mlingano, Ilonga, Tumbi Tabora, Taasisi ya Mifugo Morogoro, Ukiriguruna Chuo cha Mifugo Mpwapwa.

Kwa upande wa Uhandisi na Sayansi nyinginezo, kundilinalojumuisha vyuo vya Teknohama na Sayansi ya Kompyuta, vyuo vyenye ithibatini Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam, Chuo cha Ubaharia Dar es Salaam, MISAMbeya, Chuo cha Ufundi Arusha, Chuo cha ufundi Karume, Chuo cha Maji chaRwegarulila, Taasisi ya Ardhi Morogoro, Chuo cha Taifa cha Usafirishaji. 

Vingine ni Chuo cha Madini Dodoma, Chuo cha JR na Acharya,St Joseph cha Dar es Salaam, St Joseph Songea, Taasisi ya Kimataifa yaMawasiliano, Umeme na Kompyuta ya Kilimanjaro, Kituo cha kompyuta cha ChuoKikuu cha Dar es Salaam, Chuo cha Sukari Kidatu, Taasisi ya maendeleo ya jamiiMisungwi.

Vilivyo na ithibati ya muda ni Chuo cha Anga, Ardhi Tabora,chuo cha Learn IT na Institute for Information Technology Dar es Salaam. 

Aidha, vyuo vya kategori ya Uhasibu, Biashara na Utawala vilivyo na hadhi ya usajili kamili ni pamoja na Chuo cha Azania, TIA Mtwara, CBEMwanza, Taasisi ya Utawala wa Umma Zanzibar, na Aseki Dodoma. 

Vilivyo na usajili wa muda ni Taasisi ya Biashara Modern,RETCO Iringa, Shule ya Evin, Agape naChuo cha Biashara na Menejimenti (CBM).Kilicho katika usajili wamaandalizi ni Chuo cha Covenant chajijini Dar es Salaam.
Katika kundi la vyuo vya kilimo, maliasili na mazingira,vyuo vyenye usajili kamili ni Igarusi, Njuweni, Kilacha, Igabiro, Madaba naKizimbani Zanzibar.

Vilivyo na usajili wa muda ni Buhuri Tanga, Chuo cha Taifacha Utalii Arusha, Taasisi ya Mazingira na Masomo ya Maendeleo Dar es Salaam,Taasisi ya Maendeleo ya Utalii Zanzibar, Taasisi ya Utalii na Uongozi wa Hoteliya Victoria.
Vyuo vyenye usajili wa maandalizi ni Chuo cha Sinon na Taasisi ya Masomo yaHoteli na Biashara Dar es Salaam.

Kundi la Uhandisi na sayansi, vyuo vyenye usajili kamili niChuo cha Reli Tabora, Chuo cha Bandari, Chuo cha Suram, Techno Brain, MabughaiCDTTI na University computing centres (Arusha, Mwanza, Dodoma na ).

Vyuo vilivyo na usajili wa muda katika kundi hili ni Chuo cha Hali ya Hewa Kigoma, RegionalAviation College, Unique Computing Centre, Chuo cha Desktop, Chuo cha Mafunzoya Utafiti cha Gataraye, Chuo cha Al Maktoum, Taasisi ya Al Muntazir, Chuo chaUokoaji Dar es Salaam na United Tanzania Aeronautics College.
Kwa mujibu wa taratibuza NACTE, vyuo vilivyo na ithibati, usajili kamili na usajili wa muda ndivyovinavyoruhusiwa kudahili wanafunzi.

1 comment:

amy aman@kiluvya said...

jaribu kufatilia kabala ya kuchukua form katika chuo ukitakacho haakikisha kimesajiliwa.

KILUVYA

KILUVYA
MASHONO

UDOM

UDOM
DODOMA UNIVERSITY